Description
Hii ni mishkaki adheem kutokana na aina ya viungo vinavyotiwa na jinsi inavyochomwa. Ni mishkaki yenye asili ya Zanzibar inayotengenezwa kwa ufundi mkubwa.
Mishkaki hii inaliwa pamoja na mchanganyiko wa witu vyengine kwa pamoja vinaitwa urojo (mix) kwa wale ambao hawapendi au hawatumii mishkaki ya ng’ombe, pia inaliwa na mbogamboga pamoja na pilipili na ukwaju kukupa ladha pekee mdomoni, wengine wanakula mishkaki hii pamoja na mkate kama vile shawarma.